Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu-logo

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

United Nations

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Location:

New Rochelle, NY

Description:

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Twitter:

@HabarizaUN

Language:

Swahili

Contact:

9178215291


Episodes
Ask host to enable sharing for playback control

Jifunze Kiswahili: Maana ya neno "MKUNGUNI."

5/7/2026
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo Dkt. Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana ya neno "MKUNGUNI."

Duration:00:00:29

Ask host to enable sharing for playback control

07 MEI 2026

5/7/2026
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambapo kandoni mwa kikao cha UNPII Flora Nducha alizungumza na mshiriki kutoka Tanzania kwenye jamii ya Wamaasai mwana harakati wa haki za jamii hiyo Adam Kulet Ole Mwarabu aliyeanza kwa kumueleza kwanini mwaka huu ni wa kipekee kwa watu wa jamii za asili. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na neno la wiki.Siku ya tano tangu kuripotiwa kwa virusi vya Hanta kwenye meli ya kifahari ya Hondius kutoka Argentina na kulazimika kutia nanga nchini Cabo Verde, hii leo Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni, (WHO) Dkt. Tedros Ghebreyesus amewaambia waandishi wa habari mjini Geneva, Uswisi kuwa uchunguzi kuhusu mlipuko huo uliosababisha hadi sasa vifo vya watu 3 wakiwemo wanandoa wawili unaendelea.Tukisalia na mlipuko huo wa virusi vya Hanta, Mwakilishi wa WHO nchini Cabo Verde amesema hivi sasa meli hiyo Hondius iko njiani kuelekea visiwa vya Canary nchini Hispania, “na kwenye meli tuna daktari wa Shirika la Afya Duniani (WHO), kuna madaktari wawili wa Kiholanzi ambao wameimarisha timu, na kuna mtaalamu mmoja wa magonjwa ya mlipuko ambaye atasafiri na meli hadi bandari inayofuata ambayo ni visiwa vya Canary. Kwa sasa hakuna mtu mgonjwa kwenye meli, lakini iwapo mtu ataugua, basi kutakuwa na madaktari na vifaa vya matibabu vya kuwahudumia wakati wa safari.”Nchini Tanzania hivi karibuni ripoti ya uainishaji wa viwango vya upatikanaji wa chakula nchini humo iliyoandaliwa kwa pamoja na serikali na shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, FAO ilieleza kuwa baadhi ya maeneo ya Halmashauri za wilaya za Same, Maswa na Monduli yako katika kiwango cha tatu yaani (IPC 3).Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili na hii leo Dkt Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana ya neno "MKUNGUNI"Mwenyeji wako ni Rashid Malekela, karibu!

Duration:00:09:59

Ask host to enable sharing for playback control

Miaka 25 ya Jukwaa la Watu wa Asili Tanzania imepiga hatua kutujumuisha - Ole Kulet Mwarabu

5/7/2026
Haki ya afya kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa ni haki ya kila mtu bila kujali uko kwenye kundi au jamii gani. Huo ulikuwa ni msisitizo mwaka huu kwenye Jukwaa la jamii za watu wa asili lililokuja jamvi wiki iliyopita hapa New York Marekani. Na kandoni mwa kikao hicho Flora Nducha alipata fursa ya kuzungumza na mshiriki kutoka Tanzania kwenye jamii ya Wamaasai mwana harakati wa haki za jamii hiyo Adam Kulet Ole Mwarabu aliyeanza kwa kumueleza kwanini mwaka huu ni wa kipekee kwa watu wa jamii za asili

Duration:00:08:12

Ask host to enable sharing for playback control

Serikali ya Tanzania inajali usawa na haki kwa watu wote kupata huduma kwa usawa - Profesa Malebo

5/6/2026
Siku tano zilizopita Jukwaa la Kudumu la Umoja wa Mataifa kuhusu Masuala ya Watu wa Asili (UNPFII) limefunga pazia hapa katika makao ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani baada ya majadiliano ya takribani wiki mbili ya wadau kutoka nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kuhusu sera, mafanikio na kukabiliana na changamoto mbalimbali katika kuhudumia wananchi wao ikiwemo jamii za watu wa asili. Kwa upande wa Tanzania, mmoja wa walioshiriki ni Katibu Mtendaji wa Tume ya shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO ya Taifa la Tanzania, Profesa Hamisi Masanja Malebo.Feisal Kirwa wa idhaa hii alifanya mahojiano naye kwanza akitaka kufahamu Tanzania ina mikakati gani ya kuhakikisha watu wa asili wanajumuishwa katika huduma za afya kwa wote?

Duration:00:02:34

Ask host to enable sharing for playback control

Abiria mwingine amethibitishwa kuwa na ugonjwa wa virusi vya Hanta

5/6/2026
Imethibitishwa kuwa abiria mwingine aliyekuwa kwenye meli ya kitalii iliyohusishwa na mlipuko wa ugonjwa wa virusi vya Hanta au Hantavirus ameambukizwa ugonjwa huo, ugonjwa ambao tayari umeua watu watatu waliokuwa ndani ya meli na kusababisha tahadhari ya kimataifa iliyoratibiwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) la Umoja wa Mataifa. Assumpta Massoi na taarifa zaidi.

Duration:00:02:35

Ask host to enable sharing for playback control

06 MEI 2026

5/6/2026
Hii leo jaridani tunaangazia maambukizi wa Hantavirus, juhudi za kutokomeza Adhabu za Viboko shuleni nchini Tanzania, na ujumbe wa Profesa Hamisi Masanja Malebo kuhusu haki za watu wa asili.Imethibitishwa kuwa abiria mwingine aliyekuwa kwenye meli ya kitalii iliyohusishwa na mlipuko wa ugonjwa wa virusi vya Hanta au Hantavirus ameambukizwa ugonjwa huo, ugonjwa ambao tayari umeua watu watatu waliokuwa ndani ya meli na kusababisha tahadhari ya kimataifa iliyoratibiwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) la Umoja wa Mataifa.Siku ya Kimataifa ya Kukomesha Adhabu za Viboko huadhimishwa Aprili 30 ya kila mwaka, na mwaka huu katika maadhimisho ya siku hiyo wiki iliyopita, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto, UNICEF, nchini Tanzania kwa kushirikiana na wadau wa haki za binadamu na elimu lilizindua kampeni iitwayo ‘No Collabo’ iliyolenga kukomesha adhabu ya viboko kwa mtindo ambao walimu zaidi ya mmoja humchapa mwanafunzi viboko kwa wakati mmoja. Rashid Malekela amezungumza na wazazi mkoani Mwanza Kaskazini Magharibi mwa nchini hiyo kupata maoni yao.Siku tano zilizopita Jukwaa la Kudumu la Umoja wa Mataifa kuhusu Masuala ya Watu wa Asili (UNPFII) limefunga pazia hapa katika makao ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani baada ya majadiliano ya takribani wiki mbili ya wadau kutoka nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kuhusu sera, mafanikio na kukabiliana na changamoto mbalimbali katika kuhudumia wananchi wao ikiwemo jamii za watu wa asili. Kwa upande wa Tanzania, mmoja wa walioshiriki ni Katibu Mtendaji wa Tume ya shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO ya Taifa la Tanzania, Profesa Hamisi Masanja Malebo.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!

Duration:00:09:59

Ask host to enable sharing for playback control

UNICEF Tanzania yaongoza kampeni kukomesha adhabu ya viboko shuleni

5/6/2026
Siku ya Kimataifa ya Kukomesha Adhabu za Viboko huadhimishwa Aprili 30 ya kila mwaka, na mwaka huu katika maadhimisho ya siku hiyo wiki iliyopita, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto, UNICEF, nchini Tanzania kwa kushirikiana na wadauwa haki za binadamu na elimu lilizindua kampeni iitwayo ‘No Collabo’ iliyolenga kukomesha adhabu ya viboko kwa mtindo ambao walimu zaidi ya mmoja humchapa mwanafunzi viboko kwa wakati mmoja. Rashid Malekela amezungumza na wazazi mkoani Mwanza Kaskazini Magharibi mwa nchini hiyo kupata maoni yao.

Duration:00:03:09

Ask host to enable sharing for playback control

Jifunze Kiswahili: Maana ya methali “Kwendako mema hurudi mema."

5/5/2026
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili, leo mchambuzi wetu ni Dkt. Josephat Gitonga, ambaye ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi nchini Kenya, kwenye kitivo cha Tafsiri na Ukalimani anafafanua maana ya methali “Kwendako mema hurudi mema."

Duration:00:01:02

Ask host to enable sharing for playback control

05 MEI 2026

5/5/2026
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Kenya kumsikia kijana ambaye baada ya kukosa ajira, alichagua kujiajiri kwa kuuza miwa na juisi yake, hatua iliyomwezesha kujipatia kipato na kupambana na umaskini. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na jifunze KiswahiliShirika la Afya la Umoja wa Mataifa Duniani WHO limesema abiria na wahudumu waliokumbwa na mlipuko wa hantavirus katika meli ya utalii iliyokuwa Bahari ya Atlantiki huenda waliambukizwa virusi hivyo kabla ya kupanda meli hiyo, ingawa maambukizi miongoni mwa watu ndani ya meli hayawezi kuondolewa kabisa licha ya kuwa ni nadra. Watu saba kati ya abiria na wahudumu 147 wameugua huku wengine wakifariki dunia.Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa Duniani WHO, linaadhimisha Siku ya Kimataifa ya Usafi wa Mikono hii leo 2026 chini ya kauli mbiu “Hatua Zinazookoa Maisha,” kikisisitiza haja ya kuimarisha uzuiaji wa maambukizi katika vituo vya afya. WHO inaonya kuwa maambukizi yanayotokana na huduma za afya bado ni tishio la kila siku katika hospitali na kliniki, yakichangia usugu wa dawa za viua vijasumu au antibiotiki, ongezeko la gharama, pamoja na vifo vinavyoweza kuzuilika.Leo Mei 5 ni Siku ya Kimataifa ya Wakunga, huku Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu na Afya ya Uzazi, UNFPA, likisema wakunga ni wadau muhimu katika huduma za afya ya uzazi duniani kote. Shirika hilo linasema dunia inahitaji wakunga milioni moja zaidi ili kuboresha huduma za afya na kuokoa maisha ya wanawake na watoto wachanga. Kwa mujibu wa UNFPA, wakunga wanahakikisha ujauzito na kujifungua salama, huku pia wakisaidia kupunguza mimba zisizotarajiwa, maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto na upasuaji usio wa lazima wakati wa kujifungua.”Katika kujifunza lugha ya Kiswahili, leo mchambuzi wetu ni Dkt. Josephat Gitonga, ambaye ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi nchini Kenya, kwenye kitivo cha Tafsiri na Ukalimani anafafanua maana ya methali “Kwendako mema hurudi mema."Mwenyeji wako ni Rashid Malekela, karibu!

Duration:00:09:58

Ask host to enable sharing for playback control

Kenya tunashirikiana na mataifa jirani kutokomeza ukeketaji_ Hanna Wendot Cheptumo

5/4/2026
Ukeketaji bado ni changamoto katika maeneo kadhaa duniani na takwimu za Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani, WHO hadi mwaka jana kulikuwa na zaidi ya wasichana na wanawake zaidi ya milioni 230 walio hai waliokeketwa katika nchi 30 za Afika, Mashariki ya Kati na Asia. Kupitia mahojiano yaliyofanyika kandoni mwa Mkutano wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake Duniani, CSW70 jijini New York, Marekani, miezi miwili iliyopita, Hanna Wendot Cheptumo Waziri wa Jinsia, Utamaduni na Maslahi ya Watoto wa Jamhuri ya Kenya anaeleza hatua zinazochukuliwa na nchi yake kupambana na hali hiyo ya ukeketaji.

Duration:00:03:00

Ask host to enable sharing for playback control

WHO Afrika yawatoa hofu wananchi kuhusu Hantavirus

5/4/2026
Shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni WHO kanda ya Afrika limesemalinafuatilia kwa karibu na kutoa msaada unaohitajika tukio la afya ya umma kuhusu ugonjwa wa Virusi vya Hanta uliothibitishwa kutokea katika meli ya kitalii iliyosafiri katika Bahari ya Atlantic ambapo mpaka kufikia sasa watu watatu wamepoteza maisha. Tupate taarifa zaidi kutoka kwa Leah Mushi

Duration:00:02:28

Ask host to enable sharing for playback control

04 MEI 2026

5/4/2026
Hii leo jaridani tunaangazia ugonjwa unaotokana na virusi vya hantavirus, njaa na afya kwa raia nchini Somalia, na ujumbe wa mshiriki wa mkutano wa CSW70 Hanna Wendot Cheptumo Waziri wa Jinsia, Utamaduni na Maslahi ya Watoto wa Jamhuri ya Kenya kuhusu ukeketaji.Shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni WHO kanda ya Afrika linafuatilia kwa karibu na kutoa msaada unaohitajika kufuatia tukio la afya ya umma kuhusu ugonjwa wa Virusi vya Hanta uliothibitishwa kutokea katika meli ya kitalii iliyosafiri katika Bahari ya Atlantic ambapo mpaka sasa watu watatu wamepoteza maisha.Wanawake na watoto waliokimbia ukame na migogoro nchini Somalia wameonya kuwa wanazidi kutumbukia katika janga la kibinadamu la njaa na mateso huku kupungua kwa ufadhili wa misaada ya kibinadamu kukiendelea kuathiri maisha ya watu kote nchini humo. Onyo lao limetolewa wakati mkuu wa masuala ya dharura na misaada ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa, Tom Fletcher, akihitimisha ziara yake katika kambi za wakimbizi na vituo vya afya mjini Mogadishu na Baidoa mwishoni mwa wiki.Ukeketaji bado ni changamoto katika maeneo kadhaa duniani na takwimu za Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani, WHO hadi mwaka jana kulikuwa na zaidi ya wasichana na wanawake zaidi ya milioni 230 walio hai waliokeketwa katika nchi 30 za Afika, Mashariki ya Kati na Asia. Kupitia mahojiano yaliyofanyika kandoni mwa Mkutano wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake Duniani, CSW70 jijini New York, Marekani, miezi miwili iliyopita, Hanna Wendot Cheptumo Waziri wa Jinsia, Utamaduni na Maslahi ya Watoto wa Jamhuri ya Kenya anaeleza hatua zinazochukuliwa na nchi yake kupambana na hali hiyo ya ukeketaji.”Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!

Duration:00:09:57

Ask host to enable sharing for playback control

Janga la njaa na mateso vinazidi kutuangamiza, raia nchini Somalia wamweleza Fletcher

5/4/2026
Wanawake na watoto waliokimbia ukame na migogoro nchini Somalia wameonya kuwa wanazidi kutumbukia katika janga la kibinadamu la njaa na mateso huku kupungua kwa ufadhili wa misaada ya kibinadamu kukiendelea kuathiri maisha ya watu kote nchini humo. Onyo lao limetolewa wakati mkuu wa masuala ya dharura na misaada ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa, Tom Fletcher, akihitimisha ziara yake katika kambi za wakimbizi na vituo vya afya mjini Mogadishu na Baidoa mwishoni mwa wiki. Flora Nducha na taarifa zaidi

Duration:00:03:02

Ask host to enable sharing for playback control

30 APRILI 2026

4/30/2026
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambapo tunamsikia Dkt. Tulia Ackson, Rais wa Muungano wa Mabungeni duniani, (IPU) ambaye hivi karibuni akiwa makao makuu ya UN, Marekani aliongoza kikao kilichokuwa sehemu ya Mkutano wa CSW70. Mara baada ya kikao hicho Assumpta Massoi wa Idhaa hii ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa alizungumza naye masuala kadhaa ikiwemo yale waliyopatia kipaumbele ili kusongesha usawa wa kijinsia duniani.Karibu Dkt. Tulia.Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres hii leo saa 3 asubuhi kwa saa za New York Marekani ameeleza kuwa na wasiwasi mkubwa kuhusu suala la kufungwa kwa mlango bahari wa Hormuz wakati mzozo huko mashariki ya kati ukiingia mwezi wa tatu licha ya kuwepo kwa usitishaji mapigano aliouita kuwa ni dhaifu. Katibu Mkuu ameonya kuwa kadri hali inavyoendelea, ndivyo gharama kwa ubinadamu zinavyoongezeka, akisisitiza kuwa nchi zinazoendelea zitaathirika zaidi kutokana na madeni makubwa na kupotea kwa ajira na kuwataka wahusika wote kurejesha mara moja uhuru wa usafiri kama ilivyoainishwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kupitia Azimio namba 2817.Ripoti mpya ya pamoja iliyotolewa leo na mashirika ya Umoja wa Mataifa yanayohusika na chakula, kilimo na uchumi yakishirikiana na Tume ya Muungano wa Afrika imeonesha kuna pengo kubwa kati ya ufadhili wa sasa wa umma na binafsi wa kilimo na kiwango cha ufadhili kinachohitajika ili kubadilisha mifumo ya kilimo barani Afrika. Ripoti hiyo pia inathibitisha ongezeko linaloendelea la njaa na ukosefu wa uhakika wa chakula kote barani Afrika, ikisisitiza uharaka wa ufadhili mkubwa na endelevu ili kubadilisha mifumo ya kilimo.Na leo ni siku ya kuadhimisha muziki wa jazz duniani, siku inayotukumbusha nafasi ya muziki wa jazz kama daraja la kuleta amani, umoja na mazungumzo kati ya watu wa tamaduni tofauti. Kupitia midundo yake ya kipekee, jazz imeendelea kuwa chombo muhimu cha elimu na ushirikiano, ikiunganisha jamii duniani kote. Serikali, taasisi za elimu, mashirika ya kiraia na watu binafsi huungana kusherehekea mchango wa jazz katika kujenga jamii jumuishi.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

Duration:00:09:59

Ask host to enable sharing for playback control

Rwanda ni miongoni mwa mataifa yaliyopiga hatua kukabiliana na homa ya ini

4/29/2026
Mapambano ya kimataifa dhidi ya homa ya ini ya virusi aina ya B na C yanaanza kuonesha mafanikio, imesema ripoti mpya ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya duniani, WHO, iliyotolewa Aprili 28, 2026. Ripoti hiyo, imezinduliwa wakati wa Mkutano wa Kimataifa wa Homa ya Ini mjini Bangkok, Thailand, mkutano ulioingia leo siku ya pili na unakunya jamvi kesho. Assumpta Massoi na maelezo zaidi.

Duration:00:02:49

Ask host to enable sharing for playback control

Nimesahau yaliyopita na naganga yajayo baada ya kuuawa kwa baba yangu - Rwibutso

4/29/2026
Siku 100 za maombelezo ya kumbukumbu ya mauaji ya Kimbari ya Rwanda dhidi ya Watutsi yaliyofanyika yapata miaka 32 iliyopita zikiendelea . Leo tunakupeleka mjini Kigali nchini Rwanda kwenye Ofisi ya Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini humo kwake Eugene Uwimana afisa habari wa ofisi hiyo ili kupata simulizi ya ya kijana anayemuenzi baba yake aliyekuwa mfanyakazi wa Umoja wa Mataifa ambaye aliuawa katika mauaji hayo ya kimbari. Jina la baba huyo ni Emmanuel Turatsinze

Duration:00:02:51

Ask host to enable sharing for playback control

29 APRILI 2026

4/29/2026
Hii leo jaridani tunaangazia mkutano wa Kikanda wa Afya Barani Afrika wa mwaka 2026 unaokunja jamvi leeo, Mapambano ya kimataifa dhidi ya homa ya ini ya virusi aina ya B na C, na maombelezo ya kumbukumbu ya mauaji ya Kimbari ya Rwanda.Mkutano wa Kikanda wa Afya Barani Afrika wa mwaka 2026 “World Health Summit 2026” umehitimishwa leo mjini Nairobi nchini Kenya, ukiwaleta pamoja zaidi ya wajumbe elfu moja kutoka takribani nchi 50 kujadili namna ya kuimarisha mifumo ya afya barani Afrika na duniani.Mapambano ya kimataifa dhidi ya homa ya ini ya virusi aina ya B na C yanaanza kuonesha mafanikio, imesema ripoti mpya ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya duniani, WHO, iliyotolewa Aprili 28, 2026. Ripoti hiyo, imezinduliwa wakati wa Mkutano wa Kimataifa wa Homa ya Ini mjini Bangkok, Thailand, mkutano ulioingia leo siku ya pili na unakunya jamvi kesho.Siku 100 za maombelezo ya kumbukumbu ya mauaji ya Kimbari ya Rwanda dhidi ya Watutsi yaliyofanyika yapata miaka 32 iliyopita zikiendelea . Leo tunakupeleka mjini Kigali nchini Rwanda kwenye Ofisi ya Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini humo kwake Eugene Uwimana afisa habari wa ofisi hiyo ili kupata simulizi ya kijana anayemuenzi baba yake aliyekuwa mfanyakazi wa Umoja wa Mataifa ambaye aliuawa katika mauaji hayo ya kimbari. Jina la baba huyo ni Emmanuel Turatsinze.”Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!

Duration:00:09:58

Ask host to enable sharing for playback control

Mkutano wa WHO kuhusu mifumo ya afya katika kanda ya Afrika umekunja jamvi Nairobi Kenya

4/29/2026
Mkutano wa Kikanda wa Afya Barani Afrika wa mwaka 2026 “World Health Summit 2026” umehitimishwa leo mjini Nairobi nchini Kenya, ukiwaleta pamoja zaidi ya wajumbe elfu moja kutoka takribani nchi 50 kujadili namna ya kuimarisha mifumo ya afya barani Afrika na duniani. Anold Kayanda na taarifa zaidi

Duration:00:02:46

Ask host to enable sharing for playback control

Lenga nyota ili ukizikosa uupate mwezi asema Alinda Mashiku, Mhandisi NASA

4/28/2026
Anold Kayanda wa Idhaa hii anazungumza na Dkt. Alinda Mashiku, Mhandisi wa masuala ya anga katika moja ya Vituo vya masuala ya anga za mbali nchini Marekani, NASA. Kwa kuzingatia kuwa Umoja wa Mataifa unapigia chepuo wasichana na wanawake kupata fursa katika sayansi na teknolojia, swali la kwanza la Anold Kayanda kwa Alinda Mashiku ni ameipokeaje hatua ya hivi karibuni ambapo kwa mara ya kwanza mwanamke Christina Cochameshiriki katika timu ya wana-anga waliosafiri na kufanikiwa kuuzunguka mwezi katika eneo mbali zaidi katika anga ya mbali ambako kulikuwa hakujawahi kufikiwa na wanadamu?

Duration:00:28:18

Ask host to enable sharing for playback control

28 Aprili 2026

4/28/2026

Duration:00:11:27