
Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
United Nations
Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
Location:
New Rochelle, NY
Genres:
News & Politics Podcasts
Networks:
United Nations
Description:
Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
Twitter:
@HabarizaUN
Language:
Swahili
Contact:
9178215291
Episodes
Bila mafunzo watu tutakuwa watumaiji tu wa AI na sio wanaufaika: Hassan Mhelela
5/2/2025
Katika kuelekea siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani itakayoadhimishwa kesho Jumamosi Mei 3 ambayo mwaka huu imebeba maudhui yanayoangazia athari za Akili Mnemba au AI katika uhuru wa habari na vyombo vya habari tunazungumza na mmoja wa wanahabari wa siku nyingi ili kufahamu AI inavyoleta mabadiliko katika tasnia ya habari na vyombo vya habari hususan Afrika Mashariki ambako pia pengo la kidijitali ni kubwa. Ungana na Flora Nducha kwa undani zaidi katika makala hii.
Duration:00:05:12
Akili mnemba au AI ni sawa na upanga wenye makali pande mbili - Guterres
5/2/2025
Kuelekea siku ya kimataifa ya uhuru wa vyombo vya habari Mei 3, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amesema waandishi wa habari wanakabiliwa na hatari kila uchao huku teknolojia mpya ya akili mnemba au AI ingawa licha ya manufaa nayo pia inaibua hatari mpya kwenye uhuru wa kujieleza. Assumpta Massoi na taarifa zaidi.
Duration:00:01:50
02 MEI 2025
5/2/2025
Hii leo jaridani tunaangazia Siku ya kimataifa ya uhuru wa vyombo vya habari Mei 3 tukikuletea ujumbe wa Umoja wa Mataifa kuhusu umuhimu wake. Pia tunamulika hali ya msaada wa kibinadamu nchini Sudan.Kuelekea siku ya kimataifa ya uhuru wa vyombo vya habari Mei 3, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amesema waandishi wa habari wanakabiliwa na hatari kila uchao huku teknolojia mpya ya akili mnemba au AI ingawa licha ya manufaa nayo pia inaibua hatari mpya kwenye uhuru wa kujieleza.Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani, (WFP) tayari limeanza usambazaji wa chakula katika maeneo mbalimbali ya Sudan ambako watu wanakabiliwa na jaa huku wengine wakilazimika kuhama kambi moja hadi nyingine.Makala inamulika siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani itakayoadhimishwa kesho Jumamosi Mei 3 ambayo mwaka huu ikijikita na athari za Akili Mnemba au AI katika uhuru wa habari za vyombo vya habari. Ili kufahamu AI inavyoleta mabadiliko katika vyombo vya habari hususan Afrika Mashariki ambako pia pengo la kidijitali ni kubwa."Na mashinani fursa ni yake Volker Turk Kamishna, Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa akitoa wito wa mshikamano dunia itakapoadhimisha kesho siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
Duration:00:11:50
WFP yaongeza usambazaji wa chakula nchini Sudan japo hali bado tete
5/2/2025
Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani, (WFP) tayari limeanza usambazaji wa chakula katika maeneo mbalimbali ya Sudan ambako watu wanakabiliwa na jaa huku wengine wakilazimika kuhama kambi moja hadi nyingine. Anold Kayanda na taarifa zaidi.
Duration:00:01:50
Maoni kutoka washiriki kutoka maeneo mbalimbali waliohudhuria mkutano wa jamii za asili UNPFII
4/30/2025
Hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, mkutano wa 24 wa Jukwaa la Kudumu la Watu wa jamii za asili (UNPFII) linaendelea kujadili utekelezaji wa Azimio la Umoja wa Mataifa kuhusu haki za watu wa asili na kubaini mbinu bora za kushughulikia changamoto zinazowakabili, ukileta pamoja washiriki kutoka maeneo mbalimbali kote duniani. Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa walipata fursa ya kuzungumza na baadhi yao.
Duration:00:03:24
UNESCO: Jazz ni daraja la kudumisha amani, uhuru na mshikamano
4/30/2025
Leo tarehe 30 Aprili dunia nzima inaburudika kwa pamoja kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Jazz, Kuanzia New Orleans hadi Nairobi, Tokyo hadi Tunis, miji inawasha taa majukwaani na mioyoni kusherehekea midundo yenye ladha ya kale, ya kisasa na yenye mvuto wa kipekee. Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu , sayansi na utamaduni UNESCO linasema Jazz ni zaidi ya muziki, ni daraja la kuunganisha watu na kuleta utangamano. Flora Nducha anatupasha zaidi katika makala hii
Duration:00:04:05
Ripoti kuhusu Mpox yazitaja nchi 11 za Afrika, Ulaya, China na Amerika nao wamo
4/30/2025
Maambukizi ya ugonjwa wa mpox kutokana na aina ya virusi vya monkeypox clade Ib /ˈmʌŋ.ki.pɑks kleɪd one bee/ (MPXV) yanaendelea kuripotiwa hasa barani Afrika, ambapo mataifa kumi na moja yameripoti maambukizi ya ndani ya jamii katika kipindi cha wiki sita zilizopita. Hiyo kwa mujibu wa ripoti 51 ya Shrika la Umoja wa Mataifa la Afya Ulimwenguni, WHO kuhusu hali ya mlipuko wa mpox katika nchi mbalimbali duniani. Anold Kayanda amefuatilia ripoti hiyo na anatufafanulia kwa ufupi.
Duration:00:02:03
30 APRILI 2025
4/30/2025
Hii leo jaridani tunaangazia ugonjwa wa mpox, na walinda amabini wa Umoja wa Mataifa nchini DR Congo. Makala inamuulika siku siku ya kimataifa ya muziki wa Jazz namashinani tunasalia hapa makao maku kusikia ujumbe wa mwakilishi wa shirika la watu wa jamii za Asili.Maambukizi ya ugonjwa wa mpox kutokana na aina ya virusi vya monkeypox clade Ib /ˈmʌŋ.ki.pɑks kleɪd one bee/ (MPXV) yanaendelea kuripotiwa hasa barani Afrika, ambapo mataifa kumi na moja yameripoti maambukizi ya ndani ya jamii katika kipindi cha wiki sita zilizopita. Hiyo kwa mujibu wa ripoti 51 ya Shrika la Umoja wa Mataifa la Afya Ulimwenguni, WHO kuhusu hali ya mlipuko wa mpox katika nchi mbalimbali duniani.Huko Bunia, mji mkuu wa jimbo la Ituri, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, walinda amani kutoka Bangladesh na Indonesia, wanaohudumu kwenye ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo, MONUSCO wamepatiwa medali kwa mchango wao wa ulinzi wa raia, moja ya jukumu kubwa la ujumbe huo..Makala ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya muziki wa Jazz Flora Nducha anamulika umuhimu wa jazz maadhimisho ya mwaka ambapo maudhui yanachagiza "Amani, umoja, ubunifu na uhuru miongoni mwa tamaduni."Na katika mashinani leo fursa ni yake mshiriki jukwaa la watu wa asili hapa Makao makuu Helena Steenkamp Mwakilishi wa Shirika la Watu wa jamii za Asili Kusini mwa Jangwa la Kalahari Afrika Kusini anazungumzia alichokipata hadi sasa kwenye jukwaa hilo.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
Duration:00:11:14
Walinda amani wa UN kutoka Bangladeshi na Indonesia wapewa medali nchini DRC
4/30/2025
Huko Bunia, mji mkuu wa jimbo la Ituri, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, walinda amani kutoka Bangladesh na Indonesia, wanaohudumu kwenye ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo, MONUSCO wamepatiwa medali kwa mchango wao wa ulinzi wa raia, moja ya jukumu kubwa la ujumbe huo. Assumpta Masso amefuatilia hafla hiyo na kuandaa ripoti hii.
Duration:00:01:49
29 APRILI 2025
4/29/2025
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka katika mkoa wa Mwanza kaskazini magharibi mwa Tanzania ambapo vijana wameshika hatamu kuboresha mustakabali wao. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na mashinani tunasalia hapa makao makuu.Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa Kudumisha Amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, MONUSCO, umeikaribisha kusainiwa kwa “Azimio la Kanuni” tarehe 25 Aprili 2025 mjini Washington, D.C chini ya usimamizi wa Wizara ya mambo ya nje ya Marekani, kati ya serikali za DRC na Rwanda kwa lengo la kulinda rai ana kutekeleza azimio la Baraza la Usalama namba 2773 (2025).Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA, Juliette Touma, akizungumza na waandishi wa habri mjini Geneva kwa njia ya video kutoka mji mkuu wa Jordan, Amman, wakati kuzingirwa kwa Ukanda wa Gaza kukikaribia kuingia mwezi wa pili amesema “Mzingiro wa Gaza ni muuaji wa kimya muuaji wa watoto, wazee, na watu walioko katika mazingira magumu zaidi. Mzingiro huu unamaanisha kwamba familia nzima, watu saba au wanane wanalazimika kushirikiana kopo moja la maharagwe au njegere”.Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, FAO limezitaka nchi za Kaskazini Magharibi mwa Afrika kuongeza ufuatiliaji na kuchukua hatua za mapema kudhibiti makundi ya nzige wa jangwani. Hii ni baada ya nzige wakubwa na makundi madogo kutoka ukanda wa Sahel kuhamia maeneo ya kusini mwa Sahara, hasa katikati ya Algeria, magharibi mwa Libya, na kusini mwa Tunisia tangu Februari hadi Machi mwaka huu.Na katika mashinani fursa ni yake Maruping Onkemetse Mkurugenzi na Mwanzilishi wa Kituo cha Msaada wa Familia, shirika linaloongozwa na wanawake wa asili katika Wilaya ya Gantsi, kijiji cha Chobokwane nchini Botswana anayeshiriki mkutano unaoendelea hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa wa Jukwaa la Watu wa Asili akizungumzia alichojifunza hadi sasa.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Duration:00:11:44
AI na teknolojia za kidijitali zaweza kuwa chachu ya kuhakikisha afya na usalama kazini - ILO
4/28/2025
Leo ni Siku ya Kimataifa ya Usalama na Afya Kazini mwaka huu ikibeba maudhui “Mapinduzi ya usalama na afya Kazini: Nafasi ya Akili mnemba na teknnolojia ya kidijitali mahala pa kazi” lengo likiwa kudhihirisha nguvu ya AI na teknolojia zinapotumika vyema zinaweza kuleta mabadiliko kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kazi duniani ILO. Flora Nducha na taarifa zaidi.
Duration:00:02:58
28 APRILI 2025
4/28/2025
Hii leo jaridani tunaangazia siku ya Kimataifa ya Usalama na Afya Kazini, na juhudi za Umoja wa Mataifa za kusaidia wakulima Sudan Kusini kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi. Makala tunasalia na usalama kazini na mashinani tunakwenda nchini Kenya, kulikoni?Leo ni Siku ya Kimataifa ya Usalama na Afya Kazini mwaka huu ikibeba maudhui “Mapinduzi ya usalama na afya Kazini: Nafasi ya Akili mnemba na teknnolojia ya kidijitali mahala pa kazi” lengo likiwa kudhihirisha nguvu ya AI na teknolojia zinapotumika vyema zinaweza kuleta mabadiliko kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kazi duniani ILO.Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani WFP nchini Sudan Kusini chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Korea KOICA wanaendesha mradi wa kusaidia wananchi katika kilimo ili kujenga ustahimilivu na kupambana na utapiamlo. Tupate taarifa zaidi kutoka kwa Evarist Mapesa.Makala tunabisha hodi nchini Indonesia, taifa hili la Kusini-Mashariki mwa bara la Asia, kubwa hasa ni kumulika ni kwa vipi sekta ya uvuvi nchini humu inatekeleza kivitendo wito wa shirika la Umoja wa Mataifa la Kazi, ILO kuhusu usalama na afya Kazini. Na katika mashinani fursa ni yake Abdikani Haji Hassan kutoka kambi ya wakimbizi ya Daadab iliyoko katika kaunti ya Garissa nchini Kenya ambaye kupitia Mpango wa Prospects unaoungwa mkono na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF amejikwamua kimaisha na sasa ana ndoto ya kuenda ng'ambo ili kuendeleza ujuzi wake wa kupiga picha.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Duration:00:10:39
Kampuni Indonesia zachukua hatua kuimarisha usalama na afya pahala pa kazi
4/28/2025
Huko mashariki mwa Indonesia, kampuni za usindikaji samaki za PT Chen Woo Fisheries na PT Harta Samudra zimeongeza motisha wa kazi miongoni mwa wafanyakazi wake baada ya kuchukua hatua za kuimarisha usalama na afya pahala pa kazi. Hatua hizo ambazo zimeweka mazingira ya staha pahala pa kazi zinafuatia mradi wa pamoja wa shirika la Umoja wa Mataifa la kazi, ILO na Umoja wa Kampuni za Uvuvi na Usindikaji Samaki nchini Indonesia, AP2H1. ILOKampuni Indonesia zachukua hatua kuimarisha usalama na afya pahala pa kazi kupitia mafunzo.Je nini kilifanyika na hali sasa iko vipi? Assumpta Massoi anafafanua zaidi katika makala hii inayoletwa leo hii ikiwa ni siku ya kimataifa ya usalama na afya pahala pa kazi.
Duration:00:03:32
WFP yasaidia wananchi Sudan Kusini kupambana na mabadiliko ya tabianchi
4/28/2025
Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani WFP nchini Sudan Kusini chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Korea KOICA wanaendesha mradi wa kusaidia wananchi katika kilimo ili kujenga ustahimilivu na kupambana na utapiamlo. Tupate taarifa zaidi kutoka kwa Evarist Mapesa.
Duration:00:01:46
Chanjo imepunguza vifo na maambukizi ya malaria Kenya
4/25/2025
Ikiwa leo ni siku ya malaria duniani mwaka huu ikibeba maudhui ““Malaria inatokomezwa na sisi: wekeza upya, fikiria upya, chochea upya” shirika la afya la Umoja wa Mataifa Duniani WHO limetoa wito wa kuongeza juhudi mara dufu na kutumia kila mbinu kutokomeza ugonjwa huo hatari unaoathiri mamilioni ya watu kila mwaka na kusababisha maelfu kwa maefu ya vifo. Moja ya mbinu hizo ni chanjo ambayo nchini Kenya imeanza kuzaa matunda kama anavyofafanua mwandishi wetu wa Nairobi Thelma Mwadzaya katika makala hii.
Duration:00:03:27
Uelewa wa Hakibunifu bado ni mdogo lakini ni jambo muhimu sana ulimwenguni – Wakili Joshua Msambila
4/25/2025
Kesho Aprili 26 ni Siku ya Kimataifa ya Hakibunifu - Siku ambayo ni fursa kwa ulimwengu kukumbushwa umuhimu wa haki kwa watu wanaobuni mambo mbalimbali duniani. Ili kufahamu zaidi kuhusu Hakibunifu tumezungumza na mtaalamu wa Sheria za Sanaa na Hakimiliki, Wakili Joshua Msambila wa nchini Tanzania, kwanza anaeleza kilichomsukuma yeye kujikita katika eneo hili la sheria.
Duration:00:02:26
25 APRILI 2025
4/25/2025
Hii leo jaridani tunaangazia wakimbizi wa DRC waliokimbilia Burundi, na ujumbe wa Siku ya Kimataifa ya Hakibunifu. Makala inatupeleka nchini Kenya kuangazia ugonjwa wa malaria na mashinani tunasalia hapa makao makuu katika mkutano wa Jukwaa la watu wa asili.Mazingira ya maisha kwa wakimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC waliongia Burundi na kupelekwa katika kambi ya wakimbizi ya Musenyi si endelevu na yanatishia mustakabali wao. Msemaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR Ayaki Ito, amesema hayo leo huko Geneva, Uswisi wakati akizungumza na waandishi wa Habari kuhusu hali ya wakimbizi hao wanaoendelea kumiminika nchini Burundi.Kesho Aprili 26 ni Siku ya Kimataifa ya Hakibunifu - Siku ambayo ni fursa kwa ulimwengu kukumbushwa umuhimu wa haki kwa watu wanaobuni mambo mbalimbali duniani. Ili kufahamu zaidi kuhusu Hakibunifu tumezungumza na mtaalamu wa Sheria za Sanaa na Hakimiliki, Wakili Joshua Msambila wa nchini Tanzania, kwanza anaeleza kilichomsukuma yeye kujikita katika eneo hili la sheria.”Makala hii leo ikiwa ni siku ya Malaria duniani tunaelekea Kenya kwa mwandishi wetu Thelma Mwadzaya akiangazia juhudi zinazofanyika kupitia chanjo ili kupambana na malaria ugonjwa mbao Shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO linasema mwaka 2023 pekee ulikatili maisha ya watu 597,000 na na asilimia 95 ya vifo hivyo vilitokea barani Afrika, na sasa linataka juhudi mara dufu zifanyike ili kuutokomeza.Na katika mashinanin fursa ni yake Kulet Adam Ole Mwarabu kiongozi wa jamii ya kimaasai kutoka Tanzania anayeshiriki katika mkutano wa Jukwaa la watu wa asili kutoka hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa na anatoa wito wa maendelo, amani na utunzaji wa ardhi na mazingira kwa jamii ya asili na dunia nzima kwa jumla.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Duration:00:10:57
‘Nenda rudi’ ya wakimbizi wa DR Congo nchini Burundi mazingira ya kuishi yakiendelea kuwa tete
4/25/2025
Mazingira ya maisha kwa wakimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC waliongia Burundi na kupelekwa katika kambi ya wakimbizi ya Musenyi si endelevu huku wengine wakifanya safari za nenda rudi wakivuka mto uliosheheni viboko na mamba. Taarifa zaidi na Selina Jerobon.
Duration:00:02:02
Chata ya Umoja wa Mataifa inasongesha amani, maendeleo, urafiki na haki za binadamu - Balozi Yabesh Monari
4/24/2025
Tarehe 25 mwezi Aprili kila mwaka ni siku ya kimataifa ya wajumbe wanaowakilisha nchi zao kwenye Umoja wa Mataifa. Tarehe hiyo mwaka 1945 ndio ulianza mkutano huko San Francisco, Marekani wa wajumbe 850 kutoka nchi 50 waliopitisha Chata ya Umoja wa Mataifa ikilenga kusongesha amani, maendeleo, urafiki na haki za binadamu. Kama unavyofahamu Umoja wa Mataifa sasa umekua na idadi ya wanachama ni 193 na kila moja hupeleka wawakilishi kufanikisha utekelezaij wa malengo ya Umoja huo. Lengo la siku ni kuwatambua kwani wao ndio wamepewa jukumu la kufanikisha chata hiyo. Je wajumbe hao hufanya nini? Assumpta Massoi amezungumza na Balozi Yabesh Monari wa Kenya kwenye mada hii kwa kina.
Duration:00:06:42
Jifunze Kiswahili: Matumizi ya maneno "MKALIMANI NA MFASIRI"
4/24/2025
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili mtaalam wetu leo ni Onni Sigalla, Mhariri Mwandamizi Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA anafafanua matumizi ya maneno "MKALIMANI NA MFASIRI."
Duration:00:01:12